Usichokijua Kuhusu Muuaji wa Simba Kutoka Kagera Sugar Hamis Kiiza...Alisha Ichezea Simba na Yanga



HAMIS Kiiza (Diego) ndiye aliyebaki kwenye kumbukumbu mbaya kwenye vitabu vya Simba baada ya kuwafungia Kagera Sugar bao 1-0 na Simba kukosa alama tatu kwenye mechi tatu mfululizo.

Kiiza aliingia dakika ya 58 kuchukua nafasi ya Ally Ramadhan na ilimchukua dakika 12 pekee kuweza kuweka utofauti wa matokeo kwenye mchezo huo.

Kwa bao lake hilo mbele ya Simba, Kiiza ameweka rekodi ya kuzifunga timu zote mbili akiwa anazitumikia timu hizo kwa nyakati tofauti. Septemba 20, 2015 Kiiza akiwa na jezi ya Simba, aliwapiga Kagera Sugar ‘hat trick’ kwenye Uwanja wa Mkapa.

Kisha Januari 26 amewafunga Simba akiwa na jezi ya Kagera Sugar. Kiiza kwenye mechi hiyo aliweka rekodi ya kucheza dakika chache na kisha kutolewa nje kwa kadi nyekundu kufuatia kadi mbili za njano alizopewa kwa makosa tofauti.


Huu ni mchezo wa pili kwa Kiiza tangu atue Kagera Sugar, mchezo wake wa kwanza ilikuwa ni dhidi ya Dodoma Jiji akitoa pasi ya bao lililowapa ushindi Kagera wa mabao 2-1.

Hii ni mara ya tatu Kiiza anakuja Tanzania akitokea kwao Uganda, mara ya kwanza ilikuwa 2011- 15, akiwa anaitumikia Yanga. Alipotemwa akaenda kwao Uganda.

Kisha wakati wa dirisha dogo la msimu wa 2015-16 akasajiliwa na Simba. Simba alicheza msimu mmoja tu kisha akaondoka akiwa mfungaji bora klabuni hapo, akifunga mabao 19 katika mechi 30 za ligi.


Akiwa anaitumikia Yanga alicheza mechi 80 na kufunga mabao 56, alishawahi kucheza Free State ya Afrika Kusini, URA ya Uganda, El Hilal SC El Obeid ya Sudan, Vipers na Fasil Kanema ya Ethiopia.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad