Tafiti nyingi zilizofanywa na wataalamu ulimwenguni zimeonyesha kuwa wanaume wengi wanawapenda wanawake waliojaaliwa makalio makubwa kiasi cha kuwapatia majina tofauti kwa kulingana na ukubwa wa Makalio yao kama defence, madiaba, mpododo, sitting allowance na mengineyo.
Sio siri unapopita mitaani hasa katika barabara za miji, wengi wa wanaume “huvunja” shingo zao kuangalia makalio ya wanawake wanapopita, baadhi yao huwafuata nyuma hasa hadi anakotokomea mwanadada wakifuata kuyaangalia.
Kwa mujibu wa tafiti, imebainika kuwa ni kweli wanaume huvutiwa sana na wanawake waliojaaliwa sehemu za nyuma. hasa kunapouzwa majarida, wanaume hukodolea macho picha za wanawake wenye makalio makubwa iwe ni Nicki Minaj, Kim Kardashian, Jenipher Lopez, Vera Sidika, Hamisa Mobeto, Kajala Frida na wengineo.
Daktari Ali Hassan, ambaye ni daktari binafsi jijini Nairobi anasema Utafiti uliofanywa miaka kadhaa iliyopita na chuo kikuu Bilkent, Chuo Kikuu cha Texas, na Chuo Kikuu cha American University kilichoko jijini Beirut ulibaini kuwa kweli wanaume huvutiwa sana na wanawake waliojaaliwa sehemu za nyuma.
Hali hiyo imechangia kwa sasa wanawake wengi kuamua kwenda mbele zaidi na kufanyiwa upasuaji ili kuongeza makalio, wengine wakiamua kutumia tembe za kuongeza makalio na hata wengine wakitumia Sindano za kuchomwa kila wakataia ili kuendelea kuwa na makalio makubwa. Mfano wa wanawake hawa kwa hapa nchini Tanzania ni mwanadada Muna Love
Kuhusu masuala ya kifamilia, wanaume walioshirikishwa kwenye utafiti huo walisema kuwa, mwanamke mwenye makalio makubwa anaweza kufanya kazi kwa bidii zaidi ya mwanamke asiyekuwa na matako makubwa.
Hata hivyo ilibainika kuwa, kinachowavutia wanaume sio makalio hasa bali ni kupinda kwa uti wa mgongo unaosababisha kalio kuwa kubwa zaidi.
Wakati wa utafiti huo, wanaume walioneshwa picha za makalio ya wanawake wengi na asilimia kubwa iliwapendelea wanawake waliokuwa na uti wa mgogo uliopinda kwa kiwango cha 45.5.
Wakati kukifanyika utafiti huo, wanaume walioneshwa picha za makalio ya wanawake wengi na asilimia kubwa iliwapendelea wanawake waliokuwa na uti wa mgogo uliopinda kwa kiwango cha 45.5. Katika wanaume hao, asilimia 30 ya waliooa kila mmoja alisema ikiwa angepewa nafasi ya kuchagua tena, basi angalimchukua mwanawake mwenye makalio makubwa zaidi kuliko yule aliye naye sasa.
Ripoti ya utafiti huo pia ilisema, katika miaka ya awali mwanamke aliyeonekana kuwa na makalio makubwa alipendelewa kutokana na uwezo wake wa kubeba mizigo mgongoni na isitoshe mwanamke wa aina hiyo aliwavutia wanaume wengi na hivyo alikuwa na uwezo wa kuzaa watoto wengi.
Vilevile iliaminiwa kuwa, mwanamke aliyejaaliwa upande nyuma angeweza kustahimili uzito wa mtoto aliyebebwa tumboni na hata kutopatwa na makali ya mimba ikilinganishwa na wale wenye makalio wastani.
Hata hivyo wataalam wa maswala ya kisaikolojia wanasema hali ya mwanamke kujiona hana mvuto kwa mwanaume hadi kuamua kujiongezea makalio au sehemu yoyote ya mwili wake ni aina fulani ya kutojiamini ambayo inamfanya akatae maumbile halisi aliyopewa na Muumba