Hatimaye mwanamuziki machachari kutoka nchini Ghana, Charles Nii Armah maarufu Shatta Wale, amekubali ombi la shindano la moja kwa moja na msanii Burna Boy.
Wale ameutumia ukurasa wake wa mtandao wa twitter kuandika ujumbe wa kukubali kuingia ulingoni na Burna boy ikiwa ni pamoja na kupendekeza uwanja wa taifa wa michezo wa nchini Ghana, Accra Stadium ndio utumike kukamilisha pambano hilo.
“Oh Burna boy anataka kuzichapa na mimi moja kwa moja, sawa tuifanyie kwenye uwanja huu wa michezo wa Accra. Ikiwa wewe ni mwanaume, usije kuimba wimbo wako, wacha tufanye mtindo huru (Freestyle) Ghana – Nigeria. Niko tayari kwa hili.” Aliandika.
Vita imepamba moto, Burna Boy amvua nguo Shatta Wale
Licha ya kukubali pambano hilo Shatta Wale bado ameendelea kumshambulia Burna boy kwa maneno makali ikiwa ni pamoja na kukumbushia mambo kadhaa aliyowahi kuyashuhudia kutoka kwa Burna kipindi walichokuwa na mahusiano mazuri.
Ambapo ameikosoa vikali kauli ya Burna ya kujinadi kuwa anapesa nyingi kuliko yeye kwa kuwa, Burna aliwahi kukwama kwa kukosa pesa kiasi cha kuomba mkopo kutoka kwa rafiki yake wa karibu aitwaye Biggie.
Nakuongeza kuwa anachokiona Burna boy kama mafanikio kwake ni sawa na bure mbele yake, hivyo amemkaribisha Ghana ili aende kushuhudia kiwango cha maisha anayoishi ikiwa ni pamoja na kumuonyesha jumba lake la kifahari analomiliki.
Akiendelea kwa kusema ‘aje aone kisha ajiulize hizo pesa nimepata kwenye muziki au La.’
Pamoja na hayo Shatta Wale amesema anashangwa na kitendo cha mama mzazi wa msanii Burna Boy kukaa kimya licha ya kufahamu yanayoendelea, hali ya kuwa alishawahi kuwasaidia kipindi ambacho Burna boy alishikiliwa na jeshi la polisi nchini Nigeria.
Na kuongeza kuwa katika maisha yake yote amepambana mwenyewe tangu alipokuwa chini mpaka kufikia mafanikio aliyonayo bila ya kuwepo msaada wa mama.
“Namuheshimu sana mama Burna ila sishangazwi na Burna kutokuwa na heshima kwa sababu amekosa malezi ya baba”
Shatta wale ameonyesha kuvurugwa kwa kiasi kikubwa na kinachoendelea baina yake na Burna boy kiasi cha kutiririsha jumbe mbali mbali nzito, miongoni mwa jumbe hizo zikiwa na meneno makali yasiyofaa