Ikiwa ni baada ya kuondoshwa katika hatua ya 16 Bora ya michuano ya AFCON 2021 kwa kuchapwa 1-0 na Gambia, wachezaji wa Timu ya taifa ya Guinea wanaocheza nje ya taifa hilo wamepitiliza moja kwa moja kurudi katika mataifa wanayocheza soka la kulipwa kutokea Cameroon.
Mastaa hao wameogopa kurejea na timu hiyo nchini Guinea kama utaratibu unavyotaka kwa hofu ya kukutana na Rais wa nchi Jenerali Mamady Doumbouya.
Rais huyo aliyeingia madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi aliwaambia wazi wachezaji hao wasirejee nchini humo bila taji hilo la AFCON 2021 wakati akiwakabidhi bendera ya nchi hiyo walipokuwa wakielekea Cameroon.