Waliofariki Ajali ya Gari Mwanza Wafikia 14



Watu 14 wamefariki dunia na wengine wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha gari aina ya Toyota Land Cruiser lililokuwa limebeba waandishi wa habari na gari la abiria aina ya Hiace iliyotokea wilayani Busega mkoani Simiyu, leo Januari 11, 2022.

Mkuu wa Wilaya ya Busega, Gabriel Zakaria amezungumza na wanahabari akiwa eneo la ajali na kueleza kuwa gari ya waandishi wa habari ilikuwa na waandishi saba waliokuwa kwenye msafara wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wakielekea wilayani Ukerewe, watano kati yao wamepoteza maisha papohapo huku abiria sita nao wakipoteza maisha papohapo.

Aidha, DC Gabriel ameongeza kuwa watu wengine watatu katika majeruhi waliokuwa katika Kituo cha Afya cha Nasa, Busega wamepoteza maisha na kufanya idadi ya waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo kuwa 14.

“Nimeelezwa walikuwepo waandishi wa habari saba kutoka vyombo mbalimbali vya habari pamoja na dereva. Imeelezwa watano wamefariki eneo la tukio kutoka katika gari ya waandishi na sita wamefariki katika Hiace.

“Nimezungumza na daktari wa kituo cha Afya cha Nasa amenieleza kuwa kuna wengine watatu wamefariki kutoka katika wale majeruhi waliopelekwa hospitalini hapo.

“Hayo ni kwa sasa, sijajua nini kitaendelea kwa majeruhi wengine, polisi kwa kuwa hili ni eneo lao zaidi watafafanua, natoa pole sana kwa wote walioguswa na msiba huu,” alisema Gabriel Zakaria.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad