Waliokufa Ajali ya Boti Pemba wafikia 10

 


Zanzibar. Idadi ya watu waliopoteza maisha kwa ajali ya boti iliyotokea kisiwani Pemba imeongezeka na kufikia watu 10 huku waliokolewa wakiwa wakifikia 15.

Ajali hiyo ilitokea Januari 4 majira ya jioni wakati boti hiyo ikitokea Chakechake kwenda kisiwa cha Panza kwa ajili ya maziko ambapo moja ya boti walizokuwa wakisafiria ilipata hitilafu na kuzama.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kusini Pemba, Richard Mchonvu amesema wameopoa maiti nyingine moja hivyo kufanya idadi hiyo ifikie 10 na wengine wanne wameokolewa wakiwa hai hivyo kufanya idadi ya waliookolewa kufikia 15.

Amesema boti zilikuwa tatu zilizokuwa zikisafirisha waombolezaji kutoka Chakechake kwenda kisiwa Panza kwa ajili ya maziko ambapo boti mbili ikiwemo iliyokuwa na maiti zilivuka salama na hiyo ya tatu ilipata hitilafu kabla ya kwenda mbali kutoka kwenye gati la Chakechake.

Kamanda Mchonvu ameelezea kuwa tayari miili ya marehemu imeshakabidhiwa kwa ndugu zao baada ya kufanyiwa uchunguzi katika hospitali ya Chakechake na kukabidhiwa kwa ndugu zao.

Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo Ali Kombo alisema boti hiyo huenda ilizama kwasababu ya kujaza watuwengi maana hakukuwa na hali mbaya ya hewa wakati wanaondoka eneo hilo.

“Wala hapakuwa na mawimbi au upepo, wingi wa watu na kukosa mpangilio dani ya vyombo hivi ndio chanzo cha ajali hizi,” alisema

Chama Cha ACT Wazalendo kimetoa pole kwa familia na ndugu walioguswa na msiba huo na kuwapa pole Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi na Makamu wa kwanza wa Rais Othman Masoud katika kipindi hiki kigumu

Katibu wa Habari, Uenezi, Mawasiliano na Umma wa chama hicho, Salim Bimani amesema chama hicho kinaitaka Serikali kuimarisha vyombo vyake vya usalama ili kuleta tija yanapotokea maafa kama hayo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad