Wanaume waliopona corona hushindwa kutungisha mimba – Utafiti




Mbegu za kiume za wanaume walioambukizwa virusi vya corona huwa dhaifu kwa muda wa wiki tatu baada ya kupona.

Utafiti uliofanywa nchini Ubelgiji umebaini kuwa ndani ya kipindi hicho, waathiriwa hushindwa kutungisha mimba.

Ripoti ya utafiti huo iliyochapishwa katika jarida la Fertility and Sterility, inaonyesha kuwa mbegu za kiume za waathiriwa wanaopona hushindwa kusafiri kwenye mfumo wa uzazi wa mwanamke – hivyo, haziwezi kufikia yai la mwanamke.

Utafiti huo uliohusisha wanaume 35, waliokuwa na virusi vya corona, pia ulibaini kuwa virusi vya corona husababisha mbegu za kiume kuwa chache (low sperm count).


 
Uchache huo wa nguvu za kiume humfanya mwanaume kukosa uwezo wa kutungisha mimba.

“Wanandoa wanafaa kuelewa kwamba mbegu za kiume huwa hafifu wiki tatu baada ya mwanaume kupona virusi vya corona, Hivyo ni kazi bure kujaribu kusaka mtoto ndani ya kipindi hicho,” inasema ripoti ya utafiti huo.

Wataalamu wanaamini kuwa hali hiyo husababishwa na idadi kubwa ya kingamwili zinazozalishwa mwilini kupambana na virusi vya corona.


Idadi kubwa ya kingamwili hufanya mbegu za kiume kuwa hafifu, kwa mujibu wa watafiti hao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad