Wataalamu: Chanjo inakukwepesha Corona, ikikupata hutalazwa wodini



"Ni kosa kabisa kufikiria kwamba haina maana katika kupokea dozi za chanjo, kwa sababu kila mtu ataugua tu. Chanjo inafanikiwa katika kubadili kirusi kuwa ugonjwa rahisi, ambao unaweza kutibiwa nyumbani mara nyingi...”

Dk. Renato Kfouri; tabibu bingwa wa Watoto na Magonjwa ya Maambukizi nchini Brazil. PICHA: MTANDAO.
JANGA la maradhi corona limeshika hatua duniani hivi sasa, huku kirusi kipya aina ya omicron ndio kimeshikilia nafasi. Hapo inaongeza utata na maswali, juu ya ubora wa chanjo na inafanya kile kinacholengwa?

Kutoka katika hilo katika baadhi ya nchi kama vile Marekani, Ufaransa, Uingereza na Brazil, zinashuhudia ongezeko la maambukizi kutoka aina mpya za virusi vya delta na ya sasa omicron.

Wanasayansi, madaktari na taasisi za huduma za afya zinaendelea kutegemea aina mbalimbali za chanjo zilizokwishafanyiwa majaribio na kuidhinishwa kimataifa zinafaa kukinga watu na maambukizi.

UTATA ULIVYO

Ongezeko la maambukizi katika nchi kama vile Ufaransa na Uingereza, ufanisi wa chanjo kwa mara nyingine tena umerejea kujadiliwa kwenye mitandao ya kijamii.


 
Baadhi ya watumiaji wa nchi mbalimbali duniani wanakosoa hatua za kiserikali kudhibiti maambukizi kwa chanjo na miongoni mwa malalamiko ni maumivu ya jumla kichwani, mwilini kote, sambamba na uvimbe palikochomwa sindano mtu kujihisi kachoka, baridi na kichefuchefu.

Hata hivyo, wataalamu wa afya wanatetea kazi zao kwamba matukio mabaya kama vile damu kuganda mwilini na majeraha ya moyo (myocarditis) kuwa nadra wakisifu faida za dozi za chanjo ni kubwa kuliko athari zinazoweza kupatikana.

UFAFANUZI WA BINGWA

Daktari bingwa wa watoto na magonjwa ya maambukizi nchini Brazil, Renato Kfouri, anafafanua kinachojiri kwenye wimbi la kwanza la chanjo dhidi Covid -19, linalojumuisha chanjo kama za ‘Pfizer, AstraZeneca’ zikilenga kupunguza hatari ya mtu kuugua sana.


Kwa mujibu wa Dk. Kfouri ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Brazili la Chanjo, ni namna ya ugonjwa wenyewe, kufikia uwezekano wa kulazwa hospitalini na athari zaidi ya hapo.

"Chanjo hulinda vyema mtu dhidi ya kuugua sana na badala yake huumwa kwa kiwango cha kawaida, kidogo au hata kumfanya asipate aina za dalili zozote za Covid," anafafanua.

Anasema lengo hilo la chanjo linadhamiria mbali kuanzia kuzuia maambukizi yenyewe na hatua nyingine ya kulinda mgonjwa asiugue sana, akifafanua: “Lengo hili ni sawa na lengo la chanjo ya mafua ambayo yamekuwapo kwa miongo kadhaa.”

Bingwa huyo anasema dozi inayotolewa kila mwaka, siyo lazima izuie maambukizi ya virusi vya mafua, lakini huzuia madhara yake kwa makundi ya watu wanaoweza kuathiriwa zaidi, kama vile watoto, wajawazito na wazee.


 
Pia, anataja eneo la kuangalia mapana ya ulinzi huo dhidi ya athari za moja kwa moja kwa mfumo wa afya kupunguza maambukizi mabaya ya mfumo wa upumuaji kunakoenda sambamba na idadi ndogo ya wagonjwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi.

Takwimu za Jumuiya ya Madola zinaonyesha namna chanjo zinasaidia vyema, ikiwa na ufafanuzi hadi kufikia Novemba 2021 kuna jumla ya vifo milioni 1.1 na watu milioni 10.3 waliolazwa hospitalini nchini Marekani pekee.

Kituo cha Ulaya cha kudhibiti na kuzuia magonjwa (ECDC) na Shirika la Afya Duniani (WHO) kinakadiria watu 470,000 wenye umri wa zaidi ya miaka 60 wamenusurika katika nchi 33 kote barani Ulaya tangu chanjo dhidi ya Covid - 19 ilipoanza kutolewa.

HALI ILIVYO

Ni dhahiri kwamba maambukizi ya kujirudia ya mara kwa mara au kupatikana na maambukizi miongoni mwa watu kumeongezeka katika nyakati za hivi karibuni ni hali inayoweza kufafanuliwa kwa njia tatu.

Njia ya kwanza ni rahisi watu wa kawaida waliokusanyika na kusherehekea katika kipindi cha Mwaka mpya na Krismasi, kuongeza hatari ya kusambaa virusi vya corona.

Pili, ni takriban mwaka mmoja baada ya kupatikana chanjo katika baadhi ya maeneo ya dunia, wataalamu waligundua kwamba kinga ya mwili dhidi ya Covid - 19 baada ya kuchanjwa haidumu daima.

"Baada ya muda tumeshuhudia kwamba kiwango cha kinga kinapungua,” anatamka Dk. Kfouri, anayeongeza: “Kupungua huku kunaweza kuwa kwa kiwango kikubwa au cha chini kulingana aina ya chanjo na umri wa mtu binafsi."

"Hii inaonyesha haja ya kupata dozi ya tatu, kwanza kwa wazee na wenye kinga ya mwili ya kiwango cha chini, na baadaye kwa watu wote wazima," anafafanua daktari bingwa huyo.

Kigezo cha tatu kinatajwa kuwapo aina mpya ya kirusi omicron kuwa sugu dhidi ya chanjo za awali. Daktari huyo anaendelea: "Kutokana na suala la kwamba watu waliochanjwa hupata maambukizi linapaswa kuangaliwa kama kitu cha kawaida na tutahitajika kujifunza kuishi na hali hii."


 
"Kwa bahati nzuri ongezeko la hivi karibuni katika maambukizi ya Covid limesababisha kiwango kidogo cha watu wanaolazwa hospitalini na vifo, hususan miongoni mwa watu ambao tayari wamekwishapata chanjo.

"Chanjo inaendelea kuwalinda watu dhidi ya kuugua sana kama ilivyotarajiwa," anahitimisha.

USHAHIDI WA TAKWIMU

Chati kutoka Mfumo wa Huduma ya Afya ya New York, inaonyesha ufanisi wa chanjo unaonyesha mwanzoni mwa mwezi uliopita, idadi ya wagonjwa waliolazwa na vifo katika jiji la New York vilipanda kwa kiwango kikubwa miongoni mwa ambao hawakupata chanjo.

Pia, uwasilisho huo wa kitakwimu unaonyesha hakuna mabadiliko miongoni mwa waliochanjwa, wachache kati yao ndio walilazwa na kufariki katika shida ya kiafya inayohusiana na Covid – 19, ikilinganishwa na wasiochanjwa.

UCHAMBUZI UGHAIBUNI

Katika ripoti ya hivi karibuni, Shirika la Afya na Usalama la Uingereza, lilifafanua katika majumuishi yanayohusisha Chuo Kikuu cha Cambridge, Uingereza ikionyesha iwapo mtu ataambukizwa kirusi Covid aina ya Omicron, hatari ya kulazwa kwake hospitalini inapungua kwa asilimia 81 na anayechanjwa dozi zote tatu za kinga ya maradhi hayo.

Utafiti mwingine, unaonyesha kwamba chanjo zote tatu zina ufanisi wa asilimia 88, ingawa bado haijafahamika ni muda gani zinadumu na iwapo kutakuwa na haja ya kuchanjwa chanjo nyingine ya kuziboresha katika miezi ijayo.

Mtaalamu bingwa wa masuala ya chanjo, Dk Kfouri, anafafanua ushahidi wote unaoonyesha umuhimu wa kuchanjwa katika dhana ya kukabiliana na aina ya mpya ya virusi omicron.

"Ni kosa kabisa kufikiria kwamba haina maana katika kupokea dozi za chanjo, kwa sababu kila mtu ataugua tu. Chanjo inafanikiwa katika kubadili kirusi kuwa ugonjwa rahisi, ambao unaweza kutibiwa nyumbani mara nyingi.

"Tutatoka katika janga kwa kuchanjwa kwa watu wengi, wakiwamo watoto na heshima kwa huduma za msingi, kama vile kutumia barakoa, kuwazuia watu kuunda umati na kunawa mikono," anahitimisha mtaalamu huyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad