Waziri wa Utalii wa nchini Afrika Kusini, Lindiwe Sisulu amekana kuomba msamaha kwa rais wa nchi hiyo, Cyril Ramaphosa kwa kitendo chake cha kuikosoa mahakama.
Sisalu ametoa kauli hiyo baada ya ofisi ya rais kusema kuwa Rais Ramaphosa alikutana na kiongozi huyo mapema wiki hii na aliomba msamaha na kufuta maoni yake ya ambayo yalitajwa kuwa ni ya kuumiza.
Katika makala iliyochapishwa hivi karibuni na vyombo vya habari, Waziri Sisulu aliandika kwamba baadhi ya majaji walikuwa ni ‘Waafrika waliotawaliwa kiakili’ na kwamba katiba imeshindwa kuboresha maisha ya watu weusi wa Afrika Kusini wanaoishi katika umaskini.
Waziri Sisalu amesema bado anaendelea kusimamia kauli yake hiyo aliyoitoa na kwamba ameshtushwa na tarifa iliyotolewa.