Yasemwayo kumuhusu muamuzi mwanamke katika michuano ya AFCON



Baada ya mchezo uliosimamiwa na muamuzi mwanamke Salma Mukansanga, Mkufunzi wa timu ya taifa ya Zimbabwe Norman Takanyariwa Mapeza alisema kuwa 'alifanya vyema'.

Watu mbalimbali wakiwemo mashabiki wa soka waliokuwa wakishuhudia michuano ya AFCON walikuwa na shauku ya kumuona Bi Mukansanga akiandika historia ya kuwa mwanamke wa kwanza muamuzi katika kombe hilo la Afrika, la wanaume.

Katika uwanja wa soka wae Ahmadou Ahidjo mjini Yaounde umati wa watu ulimpigia makofi na kushangilia wakati Bi Salma Mukansanga alipopiga kipenga cha kuanzisha mechi , na mechi ilipokamilika walisifu jinsi alivyousimia, anasema Mwandishi wa BBC Yves Bucyana aliyeshuhudia mtanange huyo kati ya Warriors ya Zimbabwena Syli National ya Guinea.

Katika mazungumzo na waandishi wa habari baada ya mechi, Mkufunzi waZimbabwe alisema Mukansanga alichezesha mchezo vyema

"Nafikiri kwamba ni hatua kubwa kwa CAF kumpatia fursa mwanamke kuongoza mchezho huu."

Shabiki mwingine aliandika kwenye ukurasa wa Twitter kuhusu kazi aliyoifanya Bi Mukansanga alisema "… Tulishuhudia maambuzi mengi yaliyoibua maswali katika wiki mbili zilizopita…lakini sio leo !"
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad