Kufuatia sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali za Bunge namba 4 ya Mwaka 2021,Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi NACTE limebadilisha jina na kuanzia sasa litajulikana kama Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi NACTVET.
Katibu mtendaji wa NACTVET Dkt Adolf Rutayuga amesema Mabadiliko haya madogo yameliongezea Baraza jukumu la kurekebu na kudhibiti ubora wa Mafunzo ya Ufundi Stadi ambayo awali yalikuwa yakifanyika chini ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA.