240 wauawa Ukraine, 160,000 wakimbia




WAKATI vita kati ya Urusi na Ukraine ikiendelea kwa siku ya nne mfululizo, Umoja wa Mataifa umetoa taarifa kuwa hadi sasa jumla ya raia 240 wa Ukraine wamepoteza maisha kutokana na vita hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 27 Februari, 2022 na Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu masuala ya kibinadamu (OCHA) pia imesema jumla ya raia 160,000 wa Ukraine wameikimbia nchi hiyo.

Taarifa hiyo imekuja siku moja baada ya Jeshi la Ukraine kuchapisha kile wanachodai kuwa ni mwanzo wa hasara ya Urusi.

Kulingana na chapisho kwenye ukurasa wake wa Facebook, zaidi ya wanajeshi 3,500 wa Urusi waliohusika katika uvamizi huo wameuawa na karibu 200 kuchukuliwa wafungwa.


 
Wameongeza kuwa Urusi pia imepoteza ndege 14, helikopta 8, na mizinga 102 hadi sasa.


Rais wa Ukraine, Volodomyr Zelenskky
Hayo yanajiri wakati Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres akirejelea wito wake kwa Rais wa Urusi, Viladmir Putin wa kurejesha majeshi yake nchini Urusi.

Guterres kupitia katika mkutano wake na waandishi wa habari ameeleza hali ilivyo akisema, “tunaona operesheni za kijeshi za Urusi ndani ya eneo huru la Ukraine kwa kiwango ambacho Ulaya haijaona kwa miongo kadhaa. Siku baada ya siku, nimekuwa wazi kwamba hatua hizo za upande mmoja zinapingana moja kwa moja na Mkataba wa Umoja wa Mataifa.


“Wanachama wote wataepuka katika mahusiano yao ya kimataifa kuwa katika tishio au matumizi ya nguvu dhidi ya heshima ya eneo au uhuru wa kisiasa wa nchi yoyote, au kwa njia nyingine yoyote isiyoendana na malengo ya Umoja wa Mataifa.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad