Afisa Habari Azam FC awapa somo Young Africans




Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Azam FC Thabith Chumwi Zakaria ‘Zaka Zakazi’ ameingilia kati sakata la Malalamiko ya Waamuzi lililoibuliwa na Young Africans Jumanne (Februari 08).

Idara ya Habari na Mawasilino ya Young Africans ilifanya Mkutano na Waandishi wa Habari na kuweka hadharani namna wanavyosikitishwa na maamuzi ya baadhi ya waamuzi waliochezesha michezo yao msimu huu 2021/22.

Jana Jumatano (Februari 09), Wazee wa Young Africans nao walitilia mkazo sakata hilo, kwa kuzungumza na Waandishi wa Habari huku wakiomba kuonana na Rais Samia ili kufikisha kilio chao cha waamuzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kutokana na hali hiyo, ‘Zaka Zakazi’ amejiunga kwenye hoja hiyo kwa kuiingiza klabu yake ya Azam FC kwa madai ya kunyimwa haki na waamuzi katika michezo kadhaa, hadi kufikia hatua ya kushindwa kufikia malengo iliyojiwekea.


 
‘Zaka Zakazi’ ametumia kurasa zake za mitandao ya kijamii (Instagram na Facebook) kuendeleza mjadala huo, huku akiwataka Young Africans kuwa wapole, kwani hata Azam FC imekua ikipitia hali ya kunyimwa haki inapokua kwenye mapambano ya alama tatu za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’ ameandika: YANGA MMEELEWA AZAM FC INAKWAMA WAPI?

Nafasi moja tu ya kufunga dhidi ya Mbeya City imewaibua watu wakubwa kama waziri Mwigulu, wasemaji, wahamasishaji na wazee wa Yanga na kutaka kuonana na Rais wa nchi.


Niwakumbushe tu kwamba haya mambo @azamfcofficial inakutana nayo kila msimu.

Azam FC hupoteza alama zaidi ya 15 kila msimu kwa mambo kama haya.

Kunyimwa penati, kukataliwa magoli, kuzimwa mashambulizi na hata wapinzani kupata penati au mabao yasiyo sahihi.
Msimu huu peke yake Azam FC imekataliwa penati tano, moja ikiwa dhidi yenu Yanga.

Haya huwa yanatokea katika kipindi ambacho mbio za ubingwa zimechanganya
Mbaya zaidi wakati Azam FC inakutwa na haya, wapinzani wake kwenye mbio za ubingwa wanapata magoli kona, na mambo mengine yasiyosemekana.


 
Hebu fikiria wakati Azam FC imekataliwa penati tano msimu huu, halafu Simba wanapata penati kama ile dhidi ya Tanzania Prisons au bao kama lile dhidi ya Mbeya Kwanza.

Au nyingi Yanga mnapata penati kama ile dhidi ya Ruvu Shooting au Namungo.

Sisi tunapambana tuwakamate walioko juu yetu, lakini hawakamitiki kwa sababu ya haya mambo.
Mwisho wa msimu Azam FC inakuwa ya tatu halafu swali linakuwa, MNAFELI WAPI?

Kama sisi tungesema twende kwa Rais na kumpelekea kila kosa tunalofanyiwa kwenye huu mpira wetu, basi angetumia muda mwingi sana kuhangaika na matatizo yetu badala ya matatizo ya watanzania kwa ujumla.


Hapa ndipo Azam FC inakwama. Nadhani sasa mtakuwa mmeelewa.

Ahsanteni sana!

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad