KLABU ya Simba imesema aliyekuwa mdhamini mwenza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara (NBC Premier League), GSM wamejitoa katika udhamini huo kutokana na Simba kutokubaliana na matakwa ya mkataba huo walioingia na Bodi ya Ligi.
Haya yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally; “Kwanza tuwapongeze TFF kwa kutuletea wadhamini maana ni jukumu la kila Klabu kutafuta mdhamini wake lakini sijui ni masoko yamekuwa magumu vilabu havipati hao wadhamini lakini isitumike kama fimbo ya kutuletea kila aina ya mdhamini.
“Kwa wakati ule hawakutuelewa lakini hatimaye jana wametuelewa na baada ya kutuelewa ndio tukasema “HAKI IMESHINDA sisi tulikuwa tunapigania haki na haki hiyo imeshinda.
“Simba hatukukubaliana na ule mkataba tangu mwanzo Kwasababu tuliona hauna viashiria bora kwenye maslahi ya mpira wetu na tulijaribu kupambana lakini bahati mbaya wenzetu hawakutuelewa kwa maana ya vilabu na hii ndio shida kubwa ya mpira wetu.
“Vilabu kama tunashindwa kusimama na tukapigania haki yetu kwa pamoja tataendelea kuburuzwa, tulijaribu kuonyesha njia, wenzetu waliplay part yao sijui niite ni uoga, lakini Simba tulionyesha ujasiri wetu na uelewa wetu wa masuala ya kimkataba.
“Mwezi wa 1, 2 na 3 imepita hela haijawekwa na klabu hailalamiki bodi ya Ligi hailalamiki, Bodi ya Ligi iko pale kwa maslahi ya Vilabu, Bodi ilipaswa kumwambia TFF mbona huyo mtu haleti hela. ‘Basi Mimi nabandua logo kwenye jezi za vilabu vyangu na mabango siweki uwanjani mapaka hela iingie’ hilo halijafanyika tunakuja kusikia jana baada ya Mguto kusema.
“Tuwatoe Yanga wanaonufaika moja kwa moja na huo mkataba hivi vilabau 14 vilishindwa kujipanga vikamwambia mwenyekiti wa bodi ya Ligi kuwa hatuweki mabango hatuvai wadhamini mapaka hela iingie.
“Katika sababu nane walizotoa za kuvunja mkataba ya nane ilikuwa ni Simba, inamaana hawa watu walitaka kuidhamini Simba, Tafsiri yake ni kwamba wamedhamini vilabu 15 wakiweka mabango 4 kwenye viwanja 15 ni sawa na mabango 60. Inamaana hayo hayawatoshi mpaka wavunje mkataba kwa sababu ya Simba Sports,” amesema Ahmed.