Watu 14 wakiwemo Marubani wawili wa Tanzania hawajulikani walipo baada ya Ndege yao kuanguka baharini katika Kisiwa cha Moheli, Comoro.
Mmiliki wa Ndege hiyo Captain Mazrui Mohammed wa Fly Zanzibar ameiambia Ayo Tv walikodi ndege hiyo ndogo wiki moja iliyopita huko Comoros.
"Ni kweli ajali imetokea, ndege ilipoteza mawasiliano kama saa sita na nusu mchana katika kisiwa cha Moheli, hali ya hewa ilibadilika"
"Tuliangalia track system baada ya kuangalia tukaona imeishia sehemu kabla ya kutua na kisha tukapata habari baadaye kama saa 11 hivi kuna baadhi ya vitu vimeonekana lakini hakuna Mtu aliyepatikana hivyo hatuwezi kusema watu wamekufa kwa sababu hatujapata mwili wowote, walikuwa 14 ambapo Marubani wawili wote ni Raia wa Tanzania, hao Watu 12 siwezi kujua uraia waơ Captain Mohamed Mazrui.