Akina Halima Wakifukuzwa Uanachama Ubunge wao Utakoma



Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, amesema kuwa Bunge likipewa taarifa rasmi kuwa wabunge 19 wa CHADEMA akiwemo Halima Mdee na wenzake wamefukuzwa uanachama na chama chao basi ndipo wabunge hao watakoma kuwa wabunge wa Bunge hilo.
Kauli hiyo ameitoa hii leo baada ya kukutana na wahariri na waandishi wa habari Jijini Dodoma na kusisitiza kwamba wabunge hao 19 wa viti maalum kutoka CHADEMA ni halali na si haramu kwani wasingekuwepo bungeni kama ni haramu.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad