Alikamwe "Mambo 10 nilioyaona SIMBA vs ASEC"




1: SIMBA YA KIMATAIFA.. 🦁 NGUVU MOJA.. The Slogan Says✊ Ile ndio Faida ya kitu kinachoitwa 'Uzoefu' kwenye soka.. Kwanini?

2: Kwenye hii miaka 5 ya CAF, Simba wamekutana na situation nyingi kiwanjani. Zimewajenga sana kisaikolojia kukontroo presha zao na kubaki mchezoni pindi mambo yanapokwenda Tofauti.. Ndio Faida kubwa waliyoipata mbele ya ASEC

3: Muundo wa Timu zote 2 ulifanana walipokuwa na mpira [Wote walijenga mashambulizi kutokea chini] Lakini walipishana walipokosa mpira.. Kivipi?

4: ASEC walianza kufanya Press kwenye mstari wa kati [Mid Block] huku Simba wakipress kwenye mstari wa juu [High Press] .. Kiufundi Back Line ya Asec haikuwa comfortable na mpira.. Pressing ya Simba ilianza kuonyesha kufanikiwa since dakika ya 15. Na ni kwanini ilifanya kazi zaidi kipindi cha pili mwishoni?

5: Mosi, Kutoka kwa Sakho, Simba wakapoteza Pressing Mashine moja! Pili, Baada ya bao, Timu ikaonekana kucheza kwa tahadhari sana.. Hii ikawapa nafasi ASEC kucheza kirahisi kutokea chini.. Sub za thamani ni zile za Muhilu na Bocco! Pressing ikaongezeka kwenye High Line👏

6: Kama kuna home work, Pablo anatakiwa kuifanyia kazi kwenye uwanja wa mazoezi ni kuwapa darasa viungo wawe wawili wa chini, nini wanatakiwa kufanya timu inapokosa mpira. Bado Mkude, Kanoute hawana Link nzuri kati yao

7: KAPOMBE ✊ WHAT A PERFOMANCE! Inahitaji mchezaji mwenye moyo mkubwa kuichukua ile Penalti itakayoirejesha Timu mchezoni.. Ni mtego uliowashinda mastaa wengi duniani.

8: SAKHO.. What A Goal.. Kwa vimo vya mabeki wa ASEC inahitaji ubongo wa haraka kupiga hesabu za nini anatakiwa afanye wakati mpira ukiwa hewani.. Aliondoka uwanjani muda ambao mechi ilimuhitaji zaidi!

9: Mechi nyingine nzuri kwa Henock. Alimuweka Karim Konate kwenye mfuko wake na kumfanya atakavyo. Lile ni kosa ambalo Onyango haitaji vikao kulijutia. Kwa ubora, uzoefu wake anajua adhabu inayokuja unapoleta uzembe wa aina ile

10: Nice Job Muzamir.. Bwalya anahitaji kuimprove zaidi.. And BANDA.. Bao zuri. Nafikiri alilihitaji zaidi kubust confidence yake. Next Time, zile chance hatakiwi kuzichezea namna ile

Nb: Ikiendelea hivi, sio kulalamika tu, Wataandamana kabisa 😃
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad