Alikamwe "Mambo 10 nilioyaona Yanga vs Mbeya City"


Mambo 10 nilioyaona Yanga vs Mbeya City

1: WOW.. JUST WOW! WHAT A MATCH.. 🙌 NBC PREMIER LEAGUE katika Ubora wake! BILA shaka Tumeshuhudia moja ya mechi bora ya Ligi Kuu msimu huu! Burudani sana👏

2: Nafikiri mashabiki wa Yanga wana jambo moja kubwa la kufanya.. TOA HESHIMA KWA MPINZANI👏 Wachezaji wangefanya nini zaidi? Wamekimbia, wamepambana Lakini Mbeya City walikuwa na siku bora sana kazini!

3: Bila shaka Kocha wa Mbeya City, Mathias Lule atarudi kwenye mkoba wake wa mbinu na kujipongeza kwa mpango aliokuja nao KWA MKAPA! Wakiwa na mpira wanatawanyika kwenye 4-2-4, Bila mpira wanabana uwanja kwenye 4-4-2, Timu ikianza kupress vyema kwenye Mid Block

4: Bila shaka, kocha wa Yanga, Nabi atakuwa analia na jambo moja tu. MAJERAHA. Unahitaji wachezaji wako bora kiwanjani kushinda mechi dhidi ya Timu bora

5: Yanga walikosa 'Mamlaka' ya Bangala katikati ya kiwanja. Kwanini? Job alilazimika kwenda kulia kuziba pengo la Kibwana.. Unahitaji pia Feisal aliye Timamu kurahisisha kazi ya Mayele..

6: Wale mawinga wa pembeni wa Mbeya City, Ibrahim Selemen na Ngodya ndio walikuwa nguzo ya msingi kwenye 'Transition' 2 za Mpango wa Lule.. Moja ya mechi bora sana wameicheka👏

7: Farid Mussa chini ya kiwango chake.. Mauya akapoteza kujiamini kwenye pasi zake! Aucho akakosa 'Link' nzuri katikati ya kiwanja.. Kazi ikawa nzuri kwa AZIZ ANDAMBWILE KATIKATI YA KIWANJA🙌

8: Yanga wanaweza wasitengeneza nafasi nzuri Lakini haliondoi umahiri wa Mayele ..🙌 Katika nusu Nafasi, anageuka na kutengeneza hatari

9: Mabeki wa Kati wa Mbeya City.. Shemvuni/ Hamad Wazir HESHIMA KWAO👏 Heshima pia kwa DIDA! Alikuwa na umakini sana kwenye krosi na kupaza sauti kuipanga 'Back 4' yake

10: Well Done Mshery👏 Well Done Bangala! Moloko bado anatakiwa kuonyesha zaidi tofauti ya hatari na machachari..

Nb: Ndo tumeona Tofauti ya KUTETEMA na KUTETEMEKA😃  

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad