Aliyekuwa dereva wa rais Kenyatta aomba shamba na gari




Robert Mugo
Robert Mugo Mboi, ambaye alikuwa dereva wa rais Uhuru Kenyatta pamoja na ndugu zake wengine, sasa anasema kwamba anataka azawadiwe shamba na gari kama shukran kwa kuhudumia familia hiyo katika ikulu ya Nairobi.

Mugo aliwasafirisha Uhuru, nduguye Muhoho na dadake Nyokabi kutoka Gatundu hadi shule ya St. Mary’s asubuhi saa mbili na kuwarudisha nyumbani saa kumi au saa kumi na moja jioni.

Mzee huyo, 78, zawadi hiyo anayoidai aliahidiwa na hayati mzee Jomo Kenyatta, amabaye alikuwa rais wa kwanza wa taifa hili, ila bado hajapokea kitu chochote kutoka kwa familia hiyo mpaka sasa.


Aidha, amesema kwamba angependa kukutana na rais Kenyatta ili wazungumzie zawadi hiyo ya shamba na gari ambayo anaamini kwamba itachangia pakubwa kuwapa wajukuu wake maisha mazuri.

"Kama ingewezekana tuonane hivi itakuwa vizuri zaidi. Pia nina wajukuu wangu ambao wamefuzu ila hawana kazi, ningependa kuona wakipata nafasi za ajira,” Mugo alisema.

Mkewe mzee Mugo pia amesema kwamba shamba hilo litawaondolea changamoto ya umasikini, akiongezea kwamba wana kipande kidogo sana cha ardhi ambacho hakiwezi kukidhi idadi kubwa ya watoto wao.

Mugo anasema kwamba hajakuwa na uhusiano mzuri na rais Kenyatta akisema mara ya mwisho kukutana naye ilikuwa ni katika kampeni za  uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2017.


 
“Tulikutana huko Kianyaga, akaniuliza kama nimekutana na mamake, nikamwambia siwezi mfikia labda tu nipate kichapo. Baadaye akaniomba nambari yangu ila mpaka sasa hakuna mazungumzo yoyote yamefanyika kati yetu,” Mugo aliongezea.

Mr. Mboi,ambaye alihudumu katika kikosi cha GSU kuanzia mwaka wa 1966-1997, anaishi katika hali tete kwenye kijiji cha Gichugu

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad