Aliyemuua Dada yake Alishawahi Kuua


Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro limesema kuwa kijana Shomari Malima, aliyemuua kwa kumcharanga na mapanga dada yake aitwaye Faidhat Ibrahimu (13) kutokana na ugomvi wa kifamilia, ameshawahi pia kumuua bibi yake kutokana na imani za kishirikiana ambazo zimemfanya asishiriki tendo la ndoa.


Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi wa mkoa huo SACP Fortunatus Muslimu, ikiwa ni siku chache baada ya mwanafunzi Faidhat Ibrahimu (13) mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Mwenge iliyopo Kingolwira manispaa ya Morogoro kuuawa na Kaka yake huyo.


Kutokana na tukio hilo Kamanda Muslimu, amewataka wananchi mkoani humo kuhakikisha wanashirikiana na Jeshi hilo kutoa taarifa za migogoro kwenye familia ili kudhibiti vitendo vya mauaji.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad