Raia wa Kenya, Augustine Wanyonyi(34) amefikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kuiba Biblia kwenye supermarket Jijini Nairobi ambapo amejitetea kwamba alitaka kuhubiri neno la Mungu badala ya kujiua kutokana na changamoto za kimaisha zinazomkabili baada ya nyumba yake kubomolewa.
Augustine amesema aliiba Biblia mbili ya kwake na nyingine ya Mke wake "Niliiba Biblia ili nisome, nielewe na kuhubiri neno la Mungu badala ya kujiua kutokana na matatizo yanayonikabili, nyumba yangu imebomolewa eneo la Mukuru kwa Njenga "
Alifanya tukio hilo January 30 ambapo camera za CCTV za supermarket zilimnasa akiwa na Biblia hizo ambazo hakuzilipia, atafikiswa tena Mahakamani kwa ajili ya kupewa hukumu February 16, 2022.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE