Wachunguzi wa mauaji ya Rais wa Haiti Jovenel Moise wamesema aliyekuwa Waziri Mkuu wa Nchi hiyo ambaye kwa sasa ndiye anakaimu Urais, Ariel Henry alihuhusika na mauaji hayo na kwamba hadi sasa anamlinda Kiongozi aliyesimamia zoezi zima la utekelezaji wa mauaji hayo.
Rais Jovenel aliuawa kwa kushambuliwa na risasi akiwa nyumbani kwake July 07,2021 ambapo Wiki mbili mbele Waziru Mkuu ambaye alimteua kushika nafasi hiuo July 05,2021 akaapishwa kukaimu nafasi ya Urais.
Wachunguzi wanasema Kiongozi wa genge lililomshambulia Rais huyo anashindwa kuchukuliwa hatua kwasababu analindwa na Henry ambaye anatajwa kuhusika na mauaji hayo