Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2015, Muanzilishi wa Facebook - Mark Zuckerberg ametoka nje ya list ya matajiri 10 wakubwa wa dunia baada ya hisa za kampuni ya Meta kuzidi kushuka. Mark Zuck amepoteza zaidi ya Dola Bilioni 30 (sawa na Trilioni 69) katika utajiri wake na asilimia 12.8% ya thamani ya Meta anayoimiliki.
Thamani ya hisa moja ya Meta ilifikia Dola 237 kwa hisa moja na kupoteza zaidi ya Dola Bilioni 232 sawa na Shilingi Trilioni 536 siku ya Jumanne. Imeweka historia ya kampuni iliyoshuka ghafla duniani.
Wiki iliyopita kabla ya Ripoti za faida ya Q4 2021 ya Meta kuonyesha kushuka kwa kampuni, Zuck alikuwa nafasi ya 8 katika matajiri wakubwa duniani. Sasa hivi anashika nafasi ya 12 kwa utajiri wa Dola Bilioni 84.5 sawa na Trilioni 195 za Kitanzania.