Baada ya Kujuta Kufanya Surgery Muna Love Amuangukia Mungu "Naomba Nisaidie Yesu Katika Hali yangu"


Baada ya kupatwa na masahibu, Munalove aomba toba na kuamua kuokoka upya

"Eeeh Mungu Baba, 🙌🏻🙏🏼ninakuja kwako katika Jina la Yesu , katika Damu ya Yesu Naomba unipokee,

Naomba unisikie,

Naomba toba kwako ,

Naomba nisamehe,

katika kukata tamaa, katika maisha niliyonayo , kwakujikataa kwasababu nimekataliwa .

Eeeh Mungu Naomba Unisamehe

kwakuto kukuona wewe ,
katika jambo hili ya kwamba umeandaa jambo zuri zaidi ,

Eeeeh Mungu Unisamehe kwa kung’ang’ana , kung’ang’ania kundi ambalo linataka kuua ndoto yangu

Naomba Unisamehe Yesu

Naomba nisaidie Yesu katika hali yangu

katika Jina lako Yesu nguvu zako na uwepo wako uje kwangu tena

, sasa wakati huu fufua kwa upya ndoto yako ndani yangu

,IFUFUKE kwa damu yako Yesu , upate kuitumia katika majira yake katika Jina la Yesu ,

Naomba Unisamehe majira niliyonayo

juu ya walionikataa katika Jina la Yesu Pendo lako Yesu liendelee kunihatamia

Eeeh Bwana Yesu nakushukuru kwa ndoto uliyonipa iliniwe jibu kwa ajili ya watu wengine katika Jina la Yesu

Neema yako na kibali chako kiwe pamoja nami nisipoteze ilo jibu" ameandika Munalove

Hivi karibuni ilidaiwa surgeries za kumuongezea uzuri alizofanya mrembo huyo zimemletea shida kwa kwenda ndivyo sivyo, inadaiwa Munalove alienda kwa daktari asiye na utaalamu mkubwa kuhusu mambo y surgeries, inadaiwa alienda kwa daktari huyo sababu hakuwa na gharama kubwa tofauti na daktari aliyetaarifiwa awali ambaye gharama zake ni kubwa ujuzi mzuri anao

Baada ya hapo juzi Munalove mwemyewe aliandika ujumbe mtandaoni akiwaonya watu kuhusu kukurupuka kufanya surgeries na aliahidi ataongea zaidi baadaye juu ya suala hilo na sasa ameamua kuomba toba

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad