Baba Levo "Hakuna Msanii Atabaki Konde Gang, Mwijaku Naye Naona Vimeseji Vyake Akiomba Kazi Wasafi"

 


Kupitia U-Heard ya XXL toka Clouds FM na @soudybrown ,msanii na mfanyakazi wa Wasafi FM, @officialbabalevo amedai hakuna mtu atabaki Konde Gang hata huyo @mwijaku_01 anaona vimeseji vyake anavyo tuma usafini akiomba omba kazi. Baba Levo pia amedai ni ngumu kupinga ukweli,kama unamtusi Diamond kwenye anayo yafanya kuna muda hata ukajitazama kwenye kioo utajigundua wewe ni mwehu.

Haya yote yamekuja baada ya trending ya msanii H. Baba kumpost Diamond kwenye ukurasa wake wa Instagram,wakati inafahamika wazi kuwa ni mpinzani wake. Lakini kwa Upande wa DC wa Insta na kipenzi cha watu, Mwijaku amedai H. Baba hajawahi kuwa member wa Konde Gang,yule ni shabiki na msanii kama wasanii wengine, akimtolea mfano Timbulo. Lakini pia Mwijaku amesisitiza kuwa Konde Gang itabaki kuwa Konde Gang na wasanii wake wale wale ikiwa imara.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad