"Kaka mkubwa Prof. Jay anaumwa, kwa sasa yupo kwenye matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na anaendelea vizuri.
Kama Familia tunaishukuru sana Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, madaktari bingwa wote, uongozi mzima wa Hospitali ya Muhimbili na manesi wanaomuhudumia kaka mkubwa.
Kwa kweli wanafanya kazi ya ajabu wanamuhudumia kwa upendo mkubwa sana na wanampatia huduma nzuri sana," -Black Rhino, Mdogo wa Prof Jay.