Brad Pitt amewasilisha mashitaka dhidi ya mke wake wa zamani, Angelina Jolie, juu ya mauzo ya hisa katika shamba la mizazibu alilonunua nchini Ufaransa.
Wawili hao walinunua sehemu kubwa ya eneo la shamba la Chatto Miraval katika mwaka 2008 na kuoana katika ardhi hiyo miaka sita baadaye.
Pitt anasema mke wake wa zamani alikubali kutouza sehemu ya shamba hilo la mizabibu bila kuafikiana.
Hatahivyo, kulingana na mashitaka ya Pitt, Jolie aliuza sehemu ya shamba hilo kwa mtengenezaji wa vilevi Mrusi. Bado Bi Jolie hajatoa kauli yoyote kuhusiana na mashitaka hayo.
Nyaraka za mshataka zilizowasilishwa katika mahakama ya Los Angeles Alhamisi zilieleza kuwa Pitt alifanya kazi kwa bidii kuinua shamba hilo la mizabibu hadi kufikia kiwango cha kuwa " moja ya wasambazaji zaidi wa mvinyo duniani ."
Pitt anasema Jolie aliuza hisa zake kwa kampuni inayotengeneza vilevi vikali aina ya spiriti inayomilikiwa na mfanyabiashara wa Urusi Yuri Scheffler mjini Luxembourg bila kumfahamisha.
Jolie na Pitt walitalikiana mwaka 2016 na wawili hao walinunua makazi ya Miraval kwa Euro milioni 25.
Pitt na Angelina walichumbiana kwa miaka 10 kabla ya kuoana mwaka 2014. Mwaka 2016, Bi Jolie alimuomba Pitt amtaliki.
Mwezi Januari 2021, Jolie alimfahamisha Pitt kwa maandishi kuhusu uamuzi wake wa kuuza Sheffler, akidai kuwa alikuwa amefanya"uamuzi unaoumiza kwa moyo wa huzuni.