Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amejiuzulu nafasi yake hiyo ya Unaibu Spika ili kugombea nafasi ya uspika wa Bunge hilo katika uchaguzi unaofanyika leo Februari 1, 2022 baada ya kupitishwa na chama chake cha CCM.
Wagombea 9 ambao wamekidhi matakwa ya kisheria akiwemo Dkt. Tulia wanapigiwa kura na wabunge leo.