BREAKING NEWS: Soko jingine laungua



Moshi. Moto mkubwa ambao chanzo chake bado hakijajulikana, usiku wa kuamkia leo Februari Mosi 2022 umeteketeza sehemu ya soko la Mbuyuni lililopo katika Manispaa ya Moshi.

 Mwananchi Digital ambalo lilifika katika soko hilo saa 8:30 usiku wa kuamkia leo, lilishuhudia moto mkubwa ukiwaka eneo la ndani ya soko huku gari ya Polisi maarufu kama Washawasha ikitumika kuzima moto baada ya gari ya Zimamoto kuchelewa kufika eneo la tukio.

Gari ya Kikosi  cha Zimamoto na Uokoaji kilichopo umbali wa kilometa zisizozidi tano kiliwasili eneo la tukio takribani saa 9:20 na baadae gari la Zimamoto kutoka kiwanda cha sukari cha TPC kilichopo umbali wa zaidi ya kilometa 20 kikawasili eneo hilo takribani saa 9:50 usiku.

moto pic
Wakizungumza katika eneo ka tukio, baadhi ya mashuhuda wameelezea namna moto huo ulivyoanza polepole na baadae kuwa mkubwa huku baadhi ya wafanyabiashara wakifanikiwa kuokoa baadhi ya bidhaa.


 
Shuhuda ambae ni Mlinzi wa Soko la Mbuyuni Hassan Sulemani  amesema moto ulianza majira ya saa 7:30 usiku ambapo moto huo ulianza kwenye vibanda vya katikati ya soko.

"Tulisikia harufu nzito sana harufu ambayo aiko sawa baadae tukaona kibanda cha katikati kina waka moto tumejitahidi kwa jitihada zetu kuuzima moto ikashindikana. "

Baraka Seif ambae ni mkazi wa maeneo hayo amesema moto ulianzia kwenye vibanda amesema inawezekana chanzo cha moto ni shoti ya umeme iliyotokea kwenye soko hilo la Mbuyuni.

Soko hilo limeteketea kwa moto ikiwa imepita takribani siku 15 tangu kuteketea soko la Karume jijini Dar es Salaam

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad