Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hamis Kigwangalla, Mussa Zungu na Abdallah Ally Mwinyi wamejitosa kuchukua fomu za kuwania nafasi ya Naibu Spika wa Bunge la Tanzania kufuatia aliyekuwa naibu Spika wa Bunge hilo, Dkt. Tulia Ackson kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge.