Cameroon Ilivyopindua Meza Kibabe Mbele ya Burkina Faso, Kweli ‘Mpira Dakika 90’

 


Timu ya Cameroon imefanikiwa kushika nafasi ya tatu kwenye michuano ya AFCON kibabe zaidi baada ya kuwafunga Burkina Faso kwa jumla ya mikwaju 5 – 3.

Wenyeji hao wa michuano ya AFCON walifanikiwa kufanya ‘Comeback’ ya ajabu na kukamilisha ule usemi unaosema kuwa mpira ni dakika 90.

Kwani mpaka ya 70 walikuwa washafungwa 3 – 0 lakini wametumia dakika 15 pekee kurejesha magoli yote hayo matatu (3) kupitia kwa wachezaji wake, Stephane Bahoken 71′, Vicent Aboubakar 85′, 87′.

Na hivyo mshindi wa tatu kuamuliwa kwa matuta na kufanikiwa kuondoka na mikwaju ya penati 5 – 3 na hivyo Burkina Faso ambao walishakuwa wamepewa nafasi ya kushinda ‘game’ hiyo kuondoka vichwa chini.

Mbali na mchezo huo wa leo macho na masikio ya wapenzi wengi wa soka wameyaelekeza kwenye mchezo wa fainali hiyo ya AFCON itakayowakutanisha Senegal ya Sadio Mane dhidi ya Mafarao wa Misri chini ya Mo Salah.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad