Wachezaji wa Cameroon wakisheherekea kuchuku anafasi ya tatu ya AFCON baada ya kuwashinda Burkina Faso kwa mikwaju ya penati 5.3 mjini Yaounde siku ya Jumamosi.
Wachezaji wa Cameroon wakisheherekea kuchuku anafasi ya tatu ya AFCON baada ya kuwashinda Burkina Faso kwa mikwaju ya penati 5.3 mjini Yaounde siku ya Jumamosi.
Timu ya taifa ya Cameroon -Indomitable Lions imeibuka na ushindi na kuchukua nafasi ya tatu katika michuano ya soka la kombe la mataifa ya Afrika 2021 siku ya jumamosi baada ya kuwafunga Burkinafaso. Stallions kwa njia ya penati mabao 5-3.
Burkinafaso itabidi wajilaumu wenyewe baada ya kuongoza kwa mabao 3-0 hadi mwanzoni mwa kipindi cha pili. Lakini Cameroon waliweka historia ya kupambana kwa hali ya juu na kuumaliza mchezo huo wakiwa sare ya mabao 3-3 baada ya kusawazisha magoli yote matatu katika kipindi cha pili cha mchezo huo, kabla ya kushinda mechi hiyo kwa mikwaju ya penati.
Kwa hiyo walau Cameroon wakiwa wenyeji wa michuano hiyo wamepunguza maumivu yao ya kukosa fainali lakini wamemaliza katika nafasi ya tatu na wataweza kupanda jukwaani siku ya fainali kuchukua medali ya shaba.
Mfungaji anayeongoza hadi sasa katika michuano hiyo ni mchezaji hatari wa Cameroon Vincent Aboubakar aliingia katika kipindi cha pili na kubadilisha mambo kwa Cameroon kuwa mazuri.
Mchezaji Stéphane Bahoken alipachika bao la kwanza la Cameroon naye Aboubakar akaweka kimiani mabao mawili katika dakika ya 85 na 87 ya mchezo huo na hiyo hasa ilitokana na makosa mawili ya Golikipa wa Burkina Faso, Farid Ouédraogo, na kuupeleka mchezo kwenye penati.
Cameroon mabingwa mara tano wa kombe la mataifa ya Afrika wamemaliza katika nafasi ya tatu mwaka huu na mchezaji wao Vincent Aboubakar kwa kiasi kikubwa anatarajiwa kuchukua tuzo ya kiatu cha dhahabu kwa kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo akiwa amemaliza akiwa na magoli 8 na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza katika miaka 24 kufunga zaidi ya magoli matano katika michuano hiyo akiwapita wakongwe kama vile Samuel Eto’o wa Cameroon, Shaun Bartlett wa Afrika Kusini na Odion Ighalo wa Nigeria.
Hata hivyo rekodi ya juu ya muda wote ya ufungaji bora kwenye michuano hiyo inashikiliwa na Pierre Mulamba Ndaye, wa DRC ambaye alifunga mara tisa mwaka 1974