Chama Akabidhiwa Zigo La Lawama




KIUNGO Mzambia, Clatous Chama baada ya kurejea Simba, kocha mkuu wa kikosi hicho, Pablo Franco, amempa jukumu la kupiga penalti, faulo na kona, vitu ambavyo ndani ya timu hiyo msimu huu ni kama zigo la lawama hasa penalti.

Pablo raia wa Hispania, hivi karibuni alikasirishwa na baadhi ya wachezaji wake kushindwa kutumia vizuri kufunga penalti katika michezo ya Ligi Kuu Bara.

Simba tangu kuanza kwa msimu huu, imepiga penalti tano katika Ligi Bara pekee, kati ya hizo, moja imekuwa bao lililofungwa na Rally Bwalya dhidi ya Polisi Tanzania.


Tangu Pablo ameanza kuinoa Simba Novemba, mwaka jana, ameshuhudia vijana wake wakikosa penalti tatu dhidi ya Ruvu Shooting, Azam na Mbeya City. Penalti hizo zilipigwa na Erasto Nyoni, Bwalya na Chris Mugalu. Kabla ya hapo, John Bocco alikosa dhidi ya Biashara United.


 

Chama katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports uliopigwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa
Mkapa, Dar dhidi ya Dar City, alifunga bao kwa faulo nje kidogo ya 18.


Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra kutoka ndani ya Benchi la Ufundi la Simba, kiungo huyo alianza majukumu hayo tangu mchezo wake wa kwanza wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar uliomalizika kwa suluhu. Mtoa taarifa huyo alisema, Chama ametakiwa kupiga faulo, kona na penalti kila anapokuwa uwanjani baada ya Pablo
kuvutiwa na aina ya upigaji wake.


“Pablo amevutiwa na Chama aina ya upigaji wake wa kona, penalti na faulo, hivyo kocha amemchagua kiungo huyo
kuendelea na majukumu hayo kila anapokuwa uwanjani,” alisema mtoa taarifa huyo.



Spoti Xtra lilithibitisha hilo katika michezo mitatu ambayo amecheza kiungo huyo dhidi ya Mtibwa Sugar, Kagera Sugar na Dar City ambapo alionekana kupiga faulo na kona. Katika faulo alizopiga, moja pekee alifanikiwa kufunga, ilikuwa dhidi ya Dar City

STORI: WILBERT MOLAND | SPOTI XTRA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad