Dadake Diamond na mwanamuziki wa kike wa lebo la Wasafi, Queen Darling amevunja kimya chake baada ya kupotea kwa muda mrefu kwenye tasnia ya muziki.
Queen Darling alikuwa mwanadada wa kwanza kusajiliwa na lebo ya Wasafi ambapo alitoa vibao kadhaa kabla ya kwenda kimya.
Akihojiwa na kituo kimoja cha habari nchini Tanzania ametaja sababu zilizomfanya kuamua kukaa kimya kipindi hicho chote.
Akieleza sababu za kuwakimbia wanahabari ameeleza sababu kuu ni kuwa hana kitu kipya kwa mashabiki wake, huku akiowamba mwaka huu atakuwa anaachilia kibao kipya angalau kutuliza nyoyo zao.
“Tatizo sina kitu kipya, sina kazi mpya, kwa hivyo inshallah Mwenyezi Mungu akijalia natoa kibao kipya mwaka huu, ninavyoona mwenendo wangu na taratibu zangu, najitahidi kufanya kazi kutokana na wakati,” alisema Queen Darling.
Vilevile alizungumzia vijembe ambavyo amekuwa akipokea kutoka kwa wanamitandao kuhusu ndoa yake na safari yake ya kimuziki.
Kuhusiana na ndoa yake, alieleza kuwa anayepaswa kuulizwa swali hilo ni yule aliyeoa na si yeye anapaswa kuzungumzia suala hilo.
"Mwanamume ndiye mwenye kauli, na mara nyingi huwa naheshimu kanuni, kwa hivyo nilipewa hekima, hadi mpaka leo bado niko nayo sijapewa ruhusa ya kuongea chochote kuhusu ndoa yangu,”alisema.
Akizungumzia changamoto wanazozipitia wakewenza alieleza kuwa wakati mwanamume analeta mke mwingine nyumbani inapaswa mke wa kwanza ajiangalie na kujikagua yeye mwenyewe.
“Katika ukewenza utakapochukuliwa ama atakapoletewa mke mwenzio inabidi ujiangalie wewe ambaye ulikuwepo, kuwa ulikuwa na shinda gani tatizo gani ili mwenzio kaletwa,”