Daktari Bingwa wa Mishipa ya Fahamu "Kiti Moto Inasababisha Ugonjwa wa Kifafa"


Daktari Bingwa wa mishipa ya fahamu na utindio wa Ubongo Dr. Yusuf Jamnagerwalla amesema ulaji wa nyama ya nguruwe maarufu ‘kitimoto’ husababisha kifafa iwapo hakijapikwa vizuri.

"Ugonjwa wa kifafa unatibika, ukimwona Mtu ana dalili za kifafa asifikirie kwamba amelogwa au ana mashetani/mapepo hapo ndio kila kitu kinaharibika, ukiona dalili hizo nenda kituo cha afya na kuwaachia Wataalamu wafanye kazi yao na mgonjwa atapatiwa matibabu na madawa yapo"

"Kila Jumatatu ya pili ya Februari ni siku ya kifafa na kuna Watu zaidi ya milioni 95 wanaishi na ugonjwa wa kifafa ambapo kato yao 60% hadi 70% wako kwenye nchi masikini na Nchi zinazoendelea, changamoto kubwa ni upatikanaji wa dawa"

"Kuna uhusiano kati ya ugonjwa wa akili na kifafa lakini sio wote wenye ugonjwa wa akili wana kifafa ila dalili za ugonjwa wa akili zinafanana na za ugonjwa wa kifafa" ——— Dr. Yusuph Nyamnagerwalla. via Clouds360.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad