DEREVA wa basi la shule ameuawa kwa kupigwa risasi baada ya majambazi kuvamia msafara wa mabasi matatu huko Marakwet katika eneo la Kerio Valley Kenya.
Kwa mujibu na kamanda wa polisi kaunti ya Elgeyo Marakwet, baadhi ya wanafunzi na walimu walipelekwa katika hospitali za karibu kupata matibabu huku ikihofiwa kwamba wengine hali zao ni mbaya zaidi amesema kwamba walimu na wanafunzi walikuwa wanarejea shuleni baada ya kuhudhuria shughuli la kitaaluma.
Mashahuda waliofika kuwaokoa, wavamizi hao walimiminia risasi na kupelekea dereva wa basi hilo kuaga dunia papo hapo na kisha kuanza kurusha risasi kwa walimu na wanafunzi.