Balozi Dkt. Wilbrod Slaa amekiri kuudhika na maneno kuwa 'Mbowe si Gaidi' ambayo hutolewa na baadhi ya Wananchi kuhusu kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Freeman Mbowe
Amesema Wananchi wanatakiwa kuiachia Mahakama ambacho ni Chombo cha Haki kutoa maamuzi huku akidai kuwa haendi Mahakamani kwa kuwa kuna Sura ya Kisiasa kwa wanaokwenda kufuatilia kesi hiyo
Aidha, Dkt. Slaa ameeleza kuwa hana Chuki wala Uadui dhidi ya Mbowe kwa kuwa ameshawahi kukutana naye Uwanja wa Ndege na wakabadilishana namba japo hakuna ambaye amewahi kumpigia simu mwenzake