Dr Tulia Afichua Siri yake na Jaji Mkuu



SPIKA wa Bunge, Dk Tulia Ackson, amezidi kuweka wazi histori ya maisha yake kwa kusema Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma ndiye aliyesababisha abaki kuwa Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Dk Tulia alisema hayo wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini yaliyofanyika jijini Dodoma jana ambapo Rais Samia Suluhu Hassan alikuwa mgeni rasmi. 

Awali Dk Tulia alimshukuru Rais Samia kwa imani aliyoonesha kwake katika michakato waliyoipitia na kufanya Watanzania kupitia wawakilishi wao bungeni kumchagua kuwa Spika.

Alisema Profesa Juma ni sehemu ya kijiji cha malezi alichokieleza alipochaguliwa juzi kuwa Spika wa Bunge la Tanzania.

“Yeye ni mzazi wangu kwa maana kwamba yeye ndiye aliyekuwa mwajiri wangu nilipoanza chuo kikuu, alikuwa mwalimu wangu na yeye ndiye aliyesababisha nibaki Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kufundisha, na leo nafurahi hapa kwamba ananikaribisha nije nisema neno, asante sana baba yangu,”alisema Dk Tulia. 

Jumanne,Dk Tulia alisema bungeni Dodoma kuwa, alizaliwa na kukulia katika Kijiij cha Bulyango, wilayani Rungwe akiwa ni mtoto wa Ackson Mwansasu na mama yake, Nkundwe Mwansasu.

Alisema hayo baada ya kuchaguliwa kuwa Spika wa saba wa Bunge la Tanzania akiwa mwanamke wa pili kuongoza mhimili huo baada ya Anne Makinda aliyeongoza Bunge kuanzia Novemba 2010 hadi Novemba 2015.

Dk Tulia alikuwa Naibu Spika chini ya Spika Job Ndugai kuanzia Novemba 2015 wakati alipoteuliwa na Rais John Magufuli kuwa mbunge.

Alijiuzulu unaibu spika juzi kabla ya jana kuingia kinyang'anyiro cha uspika na kupata kura zote 376 katika uchaguzi wa Spika.

 Dk Tuila aliwaeleza wabunge kuwa, alikuzwa katika vijiji vingi na kwamba kwamba tangu alipoanza shule ya msingi hadi kuhitimu chuo kikuu alikuzwa na wengi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad