UNAAMBIWA haya ni maajabu ya dunia, nchini Australia kuna maziwa na mito yenye muonekano tofauti na ilivyozoeleka ambapo Ziwa hili la Hillier ni maarufu kutokana na maji yake kuwa ya rangi ya pink.
Ziwa hilo lipo kwenye Visiwa vya Recherche vilivyopo Australia Magharibi likiwa pembeni kabisa mwa bahari ya Hindi, na ukanda wa msitu wa kijani kibichi unaofanya kazi kama kizuizi.
Ziwa hili linasadikiwa kuwa na kiwango cha juu cha chumvi na rangi hii ya pink inatokana na maji ya chumvi kuchanganyika na sodium bicarbonate (baking soda) au vijiumbe hasa mwani unaopenda chumvi (dunaliella salina) na bakteria waridi (halobacteria) ambao huhusaindia kuzalisha rangi hiyo.
Hillier lina urefu wa mita 600 (2,000 ft) na upana wa mita 250 (820 ft) na lilizinduliwa mwandishi Matthew Flinders, mnamo Januari 15, 1802 na sasa linaitwa Flinders Peak.