Mkutano wa dharura wa shirikisho la soka ulaya UEFA umefikia maamuzi ya kuuvua uwenyeji wa fainali ya Ligi ya Mabingwa barani ulaya mji wa St Petersburg nchini Urusi kufuatia machafuko ya kivita ya Urusi dhidi ya Ukraine. na sasa mchezo huo utachezwa katika jiji la Paris nchini Ufaransa.
Saint Petersburg wamepokonywa mchezo huo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa ulaya baada ya Urusi kuivamia Ukraine na shirikisho la soka barani ulaya UEFA imethibitisha tarehe ya mchezo huo itasalia kua ile ile ya Jumamosi Mei 28, lakini eneo la tukio litahamishiwa jijini paris nchini Ufaransa katika dimba la Stade de France ambalo mara ya mwisho kuhodhi fainali ya Ligi ya Mabingwa ulaya ilikua miaka 16 iliyopita wakati Barcelona ilipoichapa Arsenal magoli 2 kwa 1.
Vilabu vyote vinne vya ligi kuu ya England vinavyo shiriki ligi ya mabingwa bado vimesalia kwenye kinyang'anyiro hicho katika hatua ya 16 bora huku Chelsea, Liverpool na Manchester City wakiongoza baada ya kushinda katika mechi za mkondo kwanza, huku Manchester United wakitoshan nguvuna Atletico Madrid baada ya kutoka sare. Michezo ya mkondo wa pili inataraji kupigwa mwezi machi itakayo amua timu zitakazo fuzu hatua ya robo fainali.