Familia ya Mwanamuziki Profesa Jay Yafunguka Baada ya Rais Samia Kusema Serikali Itagharamikia Matibabu


Familia ya Mzee Leonard Haule inamshukuru Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuelekeza Wizara ya Afya kupitia Waziri Ummy Mwalimu juu ya kugharamia matibabu ya Joseph Haule (Profesa J) kuanzia sasa.

"Kama familia tunamshukuru sana Rais Samia na tunavishukuru vyombo mbalimbali vya habari kwa ushiriki wao, mitandao ya kijamii na kwa upekee Clouds Media Group, tunawashukuru Wananchi wote walioguswa na wanaoendelea kuguswa kwa kutoa michango mbalimbali ikiwemo fedha na maombi"

"Upendo mnaouonesha kwetu kama familia ni mkubwa sana, tunaomba tumuombee Ndugu yetu kila tupatapo nafasi ili arejee kwenye afya njema, Mungu awabariki sana" ——— Alex Leonard Haule, Msemaji wa Familia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad