SAKATA la Hifadhi Ngorongoro limeendelea kuchukua sura mpya baada ya Mbunge wa Monduli (CCM), Mkoa wa Arusha, Fredrick Lowassa kuibuka akisema “Wamasai wa Ngorongoro ni Watanzania na wana haki sawa kama Watanzania wengine. Anaripoti Mwandishi Wetu, Ngorongoro … (endelea).
Aidha, amesema ana amini Serikali inayoongozwa na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassa ni sikivu.
Fredrick, mtoto wa waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema hayo leo Jumatano tarehe 16 Februari 2022 kupitia ukurasa wake wa Instagram mipindi ambacho kumekuwa na mvutano hasa wa kutakiwa jamii ya wafugani ambao ni Wamasai kuondoka.
Fredrick amesema, tofauti kubwa ni kabila letu kulinda utamaduni wetu ambao pia umekuwa kivutio kikubwa cha utalii ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro.
“Naamini Watanzania wote tunafahamu heshima hii ya Ngorongoro Crater kama moja ya maajabu ya dunia na mtaji mkubwa sana kiuchumi kwa nchi yetu.”
“Nadhani ni muda sahihi sasa kwa Serikali kuiwezesha Mamlaka ya Hifadhi ya NgoroNgoro ili kulinda hifadhi yetu na kurejesha mahusiano mazuri ya wanyama na binadamu kama ambavyo imekuwa tangu kuanzishwa kwa hifadhi hii mwaka 1959,” amesema na kuongeza:
“Hoja ya wingi wa mifugo na zozote zingine zinajadilika kukiwa na mahusiano mazuri na wananchi. Tunaiamini Serikai ya Mama Samia Saluhu Hassan ni sikivu.”
Jumatatu ya tarehe 14 Februari 2022, Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa alikwenda kuzungumza na
wadau wa uhifadhi kwenye kikao kilichofanyika Wasso-Loliondo.
Alisema Serikali itaangalia utaratibu utakaofaa kuhusu suala la uhifadhi katika eneo la Loliondo lililopo kwenye wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha.
“Katika mjadala wetu, mmetoa maoni nasi tumeyapokea. Bado Serikali inayaangalia maslahi mapana ya umma. Tutawashirikisha pia ni lipi lina maslahi mapana kwa Watanzania,” alisema .
Alisema Serikali imepokea maoni waliyoyatoa, yatayojumuishwa na kuyawasilishwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan.