Msemaji wa Yanga @hajismanara Jumatatu hii amelamba dili la ubalozi wa kampuni ya pikipiki ya Hero MotoCorp inaongoza kwa kutengeneza na kuzalisha pikipiki zinazoongoza kwa ubora duniani ambapo amedai anakwenda kubadili maisha ya madereva bodaboda.
Kampeni hiyo imekuja na msemo(tag line) ya “PIGA GIA BARABARA ISHANGAE” inayoelezea ubora wa piki zilizotengenezwa kwa ajili ya miundombinu ya Tanzania. Kila pikipiki inajulikana kwa jina maarufu kutokana na sifa zake kwa mfano, Hunter 100 CC ni maarufu kama “Chombo ya Kijanja” kwa ajili ya mfumo Rafiki wa “push to start” unaomwezesha mtumiaji kuwasha bila wasiwasi. Hunter 125 CC ikijulikana kama “Chombo ya Mishe” na 150 CC inafahamika kama “Chombo ya Kibabe” kutokana na kuwa na injini kubwa kushinda pikipiki nyingine nchini.
Pikipiki hizo zinapatikana nchini nzima kwa mawakala waliosajiliwa. Mpaka leo wana wakala 27 na wanaendelea kusajili. Kwa kila pikpiki utakyo nunua unapata kofia ngumu(helmet) mbili za bure, warranty ya KM 50,000 au mwaka mmoja, bima hadi million 5 yakumkinga dereva atakapo pata ajali na service tatu za mwanzo BURE.
Kampuni ya Hero MotoCorp inaongoza kwa kutengeneza na kuzalisha pikipiki zinazoongoza kwa ubora duniani ambapo kwa Hunter 100CC inauzwa kwa Sh milioni 2.45, na Hunter 125CC- inayouzwa kwa Sh milioni 2.50 huku Hunter 150CC ikiuzwa kwa Sh millioni -2.90. Pamoja na hayo kuna fursa za mikopo kwa wanaohitaji.
“Vipuri vya pikipiki hizi vinapatikana kila kona ya nchi kwa ajili ya kuwawezesha wateja wetu kuwa na uhakika wa kufanya matengenezo na niwasihi watanzania kununua na kutumia aina hizi za pikipiki, kwanza bei zake ni rafiki na matumizi yake ni poa zaidi” alisema Afisa Operesheni Mkuu wa Sunbeam Auto Ltd Vinaykant Chaturvedi
Showroom ya HERO iliopo kisutu pembeni na Peacock hotel, ambapo jana katika uzinduzi wa duka lao hilo pia alikuwepo mdau maarufu wa soka nchini Haji Manara ambaye alisisitiza kuwa kutokana na ubora na ufanisi wa pikipiki hizo ni wazi kuwa zitawawezesha vijana kujipatia kipato zaidi na kuwataka kuzinunua.
Alisema”hakika hizi ni pikipiki bora kabisa kwa matumizi na niwasihi kuzinunua. Kwanza bei zake ni nzuri na hata kwa upande wa matumizi ya mafuta yani zinatumia mafuta poa kabisa. Hivyo ni muda sasa wa kuhamia huku na kutoka kule kwengine.”