Harmonize Aanika Yote ya Konde Gang "Narudi Mwanza"




RASMI imejulikana wazi sababu za msanii H Baba kujitenga na Konge Gang chini ya CEO Harmonize, ni kutokana na sauti ya msanii huyo kunaswa akidai kwamba tangu kutoka kwa wimbo wa Attitude alioimba na Harmonize, hajawahi kupewa hata senti moja kutoka kwenye mapato ya wimbo huo.


Haya yote yamekuja baada ya trending ya msanii H. Baba kumpost Diamond kwenye ukurasa wake wa Instagram, wakati inafahamika wazi kuwa ni mpinzani wake.


H Baba amesema kuwa amefungiwa hata shoo na hawezi ku-perform wimbo huo na kwamba pesa kubwa ambayo amewahi kupewa na bosi wake Harmonize ni Tsh milioni 2 kwa ajili ya kupanga nyumba ya kuishi huku aki akionyesha kushangaa unapangaje Dar es Salaam kwa Ths milioni 2, pesa hiyo hiyo ununue vitu vya ndani.

H. Baba ameendela kuongea kuwa ametumia pesa nyingi kumpigania Harmonize lakini hajawahi pata faida huku akidai kuna siku alipewa Tsh 20,000 mbele za watu na kubwa zaidi lililomuuma H. Baba ni Harmonize kuwahi kumtamkia kuwa ana tamaa na si kwamba Harmonize hana pesa, bali ana roho ya uchoyo.


Msukuma huyo amegusia kutokuwepo kwenye orodha ya wasanii watakaofanya performance kwenye tamasha la Afro East Carnival.

“Nashangaa kutokuwepo, ukizingatia nilijichukulia kama mimi mtu wa muhimu wa msanii mwenzangu, kwenye orodha mbili zote nimetemwa, sasa nimechoka kuteseka na nimeamua kurudi Mwanza kwa kuwa nina kila kitu huko kuanzia nyumba na magari kuliko kuendelea kupanga Dar bila maslahi,” amesema H Baba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad