Harmonize ameweka wazi masuala ya umiliki wa wimbo wa “OMOYO” ambapo amesema hana umiliki wowote kwenye wimbo huu na mapato yote yanakwenda kwa Mchungaji Jane Misso.
Konde Boy ameongeza kwa kusema licha ya kutumia gharama zake kwenye Audio na Video, hatachukua hata asilimia 1 kwenye wimbo huo, lengo ni kumuona Jane Misso akiwa amerejesha furaha yake na kung’aa kwa baraka za Mungu.
Harmonize ameandika haya: "Achilia Mbali Mapenzi Yangu Kwa Huu Wimbo ..!!! Hii Project ni Kama Zawadi Kwa Wakina Mama Wote Duniani ..!!! Hasa Wanao Mtegemea Mungu Taarifa Licha Ya Kusimamia Ghalama za RECORDING AUDIO & VIDEO Sina Umiliki wa Huuu Wimbo Hata Kwa 1% Huuu Wimbo Still Unamilikiwa na Mwenyewe MCHUNGAJI @jane_ebeneza_misso Furaha Yangu Ni Kumuona Mama Akiwa Amerejesha Furaha Yake na Kung'aa Kwa Barakha Za Mungu Na UPENDO WENU USIO NA KIPIMO kwa Mama ..!!!! ENDELEA KUTAZAMA LINK KWENYE BIO YAKE @jane_ebeneza_misso & @kondegang TUKUTANE TABATA SHULE @afroeastcarnival 🗞🗞🗞 "