Harmonize "Juma Jux ni Kaka Yangu ni Miss Understanding tu ikitokea"




Moja ya maswali yaliyoulizwa leo kwenye press ya @harmonize_tz ni kuhusu malalamiko ya @juma_jux kuwekwa kwenye list ya watakao-perform kwenye Afro East Festival bila makubaliano kufikiwa inavyotakiwa ambapo haya ndio majibu ya Harmonize.

"Jux ni Brother amekuwa kwenye Muziki kwa muda mrefu, Mimi nimekuwa Shabiki yake napenda Muziki wake, hizo miss understanding zilitokea kutokea kwa Management watakaa kulimaliza, halikuwa na haja ya kwenda kwenye media”

“Japo naheshimu uwepo wa media lakini sio kila kinachotokea kinatakiwa kuwa public maana kukiwa na mikwaruzano wakati mwingine inawakatisha tamaa wale wenye Taasisi zinazo-support Muziki, Serikali na Wadau tutaonekana Wasanii hatujielewi”

“Nirudie nirudie kusema sisi ni Ndugu hatuwezi kugombana sisi ni wamoja ni Watanzania, tusitengeneze mikwaruzano, nitahakikisha sitogombana na Kaka zangu” ——— Harmonize. #MillardAyoUPDATES

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad