Hatimaye Bernard Morisson Aomba Radhi Simba SC "Nimeikosea Club"

 


Imeelezwa kuwa Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Bernard Morisson ametuma ujumbe kwenye kundi la WhatsApp la wachezaji wa timu hiyo akiomba radhi kwa kilichotokea.

Morrison pia ametuma ujumbe huo kwa kila kiongozi wa Simba SC kwa njia hiyo ya mtandao, huku akisisitiza msamaha, ili aweze kurejeshwa kwenye kikosi cha klabu hiyo.

Kiungo huyo alisimamishwa Simba SC juma lililopita, kufuatia utovu wa nidhamu wa kutoroka kambini, hali ambayo ilipelekea Uongozi wa Simba SC kumtaka ajieleze kwa njia ya Barua kupitia kwa Afisa Mtendaji Mkuu Barbara Gonzalez.

Ujumbe wa Morisson alioutuma kwenye kundi la wachezaji wa Simba SC na kwa kila kiongozi wa klabu hiyo unasomeka: “Naomba radhi kwa wachezaji, kocha, meneja, kapteni na wachezaji wazoefu na kila mmoja aliyepo humu.”

“Naomba radhi sana kwa yale yote yanayoendelea na yaliyotokea kwani naamini nimefanya jambo la kutowaheshimu kila mmoja wenu, najua nimeikosea klabu na sikulenga kufanya hivyo,”

“Lakini kwa jambo lililotokea haina maana kwangu kujielezea binafsi naomba msamaha kutoka kwenu wote, naomba msamaha kwenu, John Bocco, Aishi Manula, Erasto Nyoni, Pascal Wawa, Joash Onyango, Clatous Chama siwezi kuwataja Wote hapa, ila naomba kwenu wote mnisaidie kuomba radhi kwa kocha na Bodi ya Wakurugenzi.”

“Nina imani baada ya hapo nakwenda kufanya vitu vilivyokuwa bora natamani amani iwepo pamoja na upendokwa mara nyingine tena. Naomba mnisamehe jamani. Nimekosa.”

Morisson alisajiliwa Simba SC mwanzoni mwa msimu wa 2020/21 baada ya kumaliza mkataba wake na Young Africans, lakini uhamisho wake ulizua utata na kupelekea kufunguliwa kesi katika Mahakama ya usuluhishi wa michezo duniani ‘CAS’.

Msimu uliopita (2021/21) Morisons alikua sehemu ya kikosi cha Simba SC kilichotwaa ubingwa wa Tanzania Bara, Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ na kufika hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad