Ubalozi wa Tanzania, Stockholm umetoa ushauri kwa Watanzania waishio Ukraine kuwa kama wanadhani kukaa kwao Ukraine siyo muhimu kwa sasa, waondoke nchini humo kutokana na kuwepo kwa hali tete ya kiusalama na kusasabisha mashaka juu ya usalama wao.
Pia umewataka wazazi wenye watoto wanaosoma nchini humo kufanya taratibu binafsi za kuwarudisha watoto wao nyumbani kwa kutumia ndege binafsi zinazofanya safari kutokea Ukraine.
Dar24 Media imezungumza na Mkurugenzi wa Habari wa Wizara ya Mambo ya Nje, Emmanuel Buhohela, amesema kuwa Wizara imemuagiza Balozi wa Sweeden kufuatilia usalama wa watanzania wote wanaoishi Ukraine.
Hata hivyo Buhohela amesema kuwa taarifa kamili kuhusu usalama na namna ya kuwanusuru watanzania wa Ukraine itatolewa kesho Februari 25.