Huyu Diamond Platnumz Unaemjua Wewe Anavaa Miwani ya Shilingi Milioni Nane



SUPASTAA mkubwa wa muziki barani Afrika, Diamond Platnumz ametamba kununua miwani ya bei mbali ya zaidi
ya shilingi milioni 8 za Kitanzania kutoka kwa dizaina maarufu duniani.

Diamond ametoboa siri hiyo baada ya kuachia vipande vya video vikimuonesha akinunua miwani kwenye duka la bling’ibling’I huko nchini Marekani.

Pia ameonesha risti aliyonunulia miwani hiyo ikionesha wazi kuwa amenunua pea tisa za miwani.

Miwani hiyo inaonesha nembo za kampuni kubwa za urembo duniani za Dolce & Gabbana, Gucci, Dior na Prada.

Miwani hiyo imemgarimu Diamond Dola za Kimarekani 3,510 (zaidi ya shilingi milioni 8,073,000 za Kitanzania.

Baada ya manunuzi hayo ameandika; “Najua unajua huwa sivai miwani feki…” Mbali na miwani hiyo, Novemba, mwaka jana, Diamond alionesha cheni na pete za madini mbalimbali ambavyo alidai vinagharmi shilingi milioni 111 za Kitanzania. Ukiacha hivyo, Oktoba, mwaka jana, Diamond alinunua saa ya bei mbaya aina ya Rolex.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad