Imebainika H Baba Ametembeza Unfollow Kwa Harmonize Kisa Kutokuwepo Kwenye List ya Tanasha Tabata



Kiukweli imekuwa ghafla sana kwa msanii H.Baba ambaye wengi wanamuona kwenye nafasi ya Uchawa kwa msanii @harmonize_tz ,kumkubali Diamond Platnumz mtu ambaye alikuwa anamkosoa kwa kila hatua ambayo Simba anapiga kwenye harakati zake za kimuziki na maisha kiujumla.

Ukipita kwenye ukurasa wa Instagram wa msanii H. Baba,ukiachana na kumpost kwa sana Diamond,lakini katembeza Unfollow kwa Harmonize na akamfollow Diamond na kisha kumuunfollow tena. Wengi wamehusisha tukio hili na list ya wasanii watakao toa burudani kwenye tamasha la Harmonize la Afro East Carnival, March 5 Mwaka huu. Ukitazama orodha ya wasanii hao, basi huwezi kutana na jina la H. Baba, kitendo ambacho inawezekana kikawa kimemuumiza msanii huyo na ukizingatia ni mtu aliyempigania sana Harmonize mitandaoni.

Lakini pia siku kadhaa nyuma, Harmonize akiwa XXL ya Clouds Fm alikana kuwa huwa hatumi watu kuwasema vibaya watu wengine, hivyo wakiongea, ni wao na hisia zao lakini si yeye.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad